Sunday, 15 April 2018
05:58:00
BWANA ANATAKA NINI KWAKO
Na sasa, Israeli, BWANA, Mungu wako, anataka nini kwako, ila umche BWANA, Mungu wako, na kwenda katika njia zake zote, na kumpenda, na kumtumikia BWANA, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote; 13kuzishika amri za BWANA na sheria zake, ninazokuamuru leo, upate uheri? 141 Fal 8:27; Zab 115:16; Mwa 14:19; Zab 24:1Tazama, mbingu ni mali za BWANA, Mungu wako, na mbingu za mbingu, na nchi, na vitu vyote vilivyomo. 15Tena, BWANA aliwafurahia baba zako, na kuwapenda, akawachagua wazao wao baada yao, naam, na ninyi zaidi ya mataifa yote kama hivi leo. 16Law 26:41; Yer 4:4; Rum 2:28; Efe 4:21; Kol 2:11Basi, zitahirini govi za mioyo yenu, wala msiwe na shingo ngumu. 171 Tim 6:15; Ufu 17:14; 19:16; Mdo 10:34; Rum 2:11; Zab 136:2; Dan 2:47; 2 Nya 19:7; Ayu 34:19; Gal 2:6; Efe 6:9; Kol 3:25; 1 Pet 1:17Kwa maana BWANA, Mungu wenu, yeye ndiye Mungu wa miungu, na Bwana wa mabwana, Mungu mkuu, mwenye kuogofya, asiyependelea nyuso za watu, wala hakubali rushwa. 18Zab 68:5; 146:9Huwafanyia yatima na mjane hukumu ya haki, naye humpenda mgeni, akimpa chakula na mavazi. 19Basi, mpendeni mgeni, kwa sababu ninyi wenyewe mlikuwa wageni katika nchi ya Misri. 20Mt 4:10; Zab 63:11Mche BWANA, Mungu wako, umtumikie yeye; ambatana naye, na kuapa kwa jina lake. 21Zab 22:3; Yer 17:14Yeye ndiye fahari yako, na yeye ndiye Mungu wako, aliyekutendea mambo haya makubwa, ya kutisha, uliyoyaona kwa macho yako.
0 comments:
Post a Comment
text